Luke 10:25-28

25 aWakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Isa, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

26Isa akamjibu, “Imeandikwaje katika Torati? Kwani unasoma nini humo?”

27 bAkajibu, “ ‘Mpende Bwana Mwenyezi Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote’; tena, ‘Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ ”

28 cIsa akamwambia, “Umejibu vyema. Fanya hivyo nawe utaishi.”

Copyright information for SwhKC